July 10, 2014





Uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuahirisha Ligi Kuu Bara kutoka Agosti 24 hadi Septemba 20 imemvuruga Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic.

Akizungumza kutokea kwao Croatia Logarusic amesema hakutegemea kitu kama hicho kinaweza kutokea bila ya timu kushirikishwa.
“Sijawahi kusikia, kwangu ni maajabu nab ado sijaamini," alisema Loga anayetarajia kutua nchini kesho alfajiri tayari kuanza maandalizi ya ligi.

“Huenda TFF walikuwa wanafanya utani katika jambo fulani, lakini hii si kawaida.
“Bora wangesema katika kipindi ambacho timu hazijaanza mazoezi, lakini si sasa.
“Kuna mambo mengi ya kupima hapa kama gharama na mengine. Sijui hii ni nini, siwelewi,” alisema Logarusic.
SALEHJEMBE ilipata taarifa hizo mapema kabla ya baadaye TFF kuzidhibitisha na zimeonekana kuwachanganya wadau wengi wa soka.
Sababu za TFF zinaonekana kutokuwa na nguvu hasa ile ya kupicha Kombe la Kagame ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka bila ya kuathiri ligi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic