July 27, 2014

  

Wachezaji wa Simba, kwa nyakati tofauti wamesema mazoezi ambayo hufanya ufukweni au gym chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola si mchezo.
Mmoja ameiambia SALEHJEMBE, yale mazoezi si mchezo huku akisema Matola ‘atawaua’.

Lakini kila mmoja wao akasisitiza kuwa anachofanya Matola ni faida ya kwao baadaye.
“Kweli ni mazoezi magumu sana, mfano ufukweni, wakati mwingine unajisikia kama unataka kufa, hahaha,” alisema mmoja.

Lakini mwingine ambaye ni kiungo kinda, aliungana na mwenzake na kusema mazoezi hayo ya ufukweni na gym ni makali sana.
Akasisitiza wanalijua hilo ndiyo maana wamekuwa wakifanya kwa juhudi wakijua ligi itakuwa na ushindani sana.
Matola ndiye amekuwa akiongoza mazoezi ya ufukweni na gym wakati Kocha Mkuu, Zdravko Logarusic amekuwa akiungana naye kwenye mazoezi ya jioni.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic