August 18, 2014



Ili kuondoa utata kwamba huenda nani ataanza katika mechi ya kesho ya Super Cup kati ya kipa Iker Casillas na yule mpya Kyler Navas, Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti ameweka wazi kabisa kwamba Casillas ndiye atacheza.
Navas amejiunga na Madrid baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia akiwa na Costa Rica.

Mechi hiyo ya Spanish Super Cup dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Atletico Madrid na tayari imekuwa gumzo.
“Tumejiandaa kwa dakika 180 za mechi hiyo, tutaanza na 90 halafu tutamalizia na kipande cha pili. Tunataka kufanya vizuri katika mechi zote,” alisema Ancelotti.
Makipa: "Iker ndiye atakayecheza na mengine tyatafuatia.”
Di María: "Siwezi kuzungumzia kuhusiana na Di Maria, ninahofia kuchelewa nilicholenga kuhusiana na mechi ya kesho.”
James: "Hajakosa chochote kama ilivyoelezewa, alijitahidi na tunaona msaada wake unahitajika, tunamhitaji.”
Diego López: "Hakuna aliyeamua kumuondoa Diego López, binafsi ndiye aliamua kubadili mazingira, tulikuwa na makipa wawili msimu uliopita, sawa na msimu huu. Hakuna tatizo.
Kroos: "Anaongeza kiwango cha timu, amekuwa changamoto na uzoefu wake umekuwa msaada katika kikosi chetu.”
Mfumo: "Tuna staili yetu, ile ya msimu uliopita pia msimu huu. Kwa kifupi hii ni Madrid, ileile."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic