VAN GAAL (KULIA) AKIWA NA KOCHA WA ZAMANI WA MAN UNITED, ALEX FERGUSON. |
Saa
chache baada ya Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kusema kikosi chake hakijawa
tayari kwa ajili ya Ligi Kuu England inayoanza leo, Louis van Gaal, naye
ameonya.
Van Gaal amesema kikosi chake cha Manchester United hakijaiva vizuri kama anavyotaka huku akitaja sababu kadhaa.
Moja
ya sababu alizotoa van Gaal ni kuhusiana na mabadiliko makubwa ndani ya kikosi
chake.
Pili
akasema kuna baadhi ya wachezaji waliowataka wakawakosa, hivyo wanajipanga na
walionao.
Tatu
ni kuhusiana na kubadili kwa mfumo anaotaka wautimie wa 3-4-1-2 ambao anasema
lazima utawasumbua wachezaji mwanzoni.
Van
Gaal amesem mfumo huo utawasumbua wachezaji kutokana na mabadiliko ya makocha
watatu ndani ya miezi zita had inane ikiwa ni baada ya kuondoka kwa Alex
Ferguson, akatua David Moyes na sasa yeye.
Tayari
suala hilo amelifikisha kwa familia ya Glazer ambao ndiyo wamiliki wa Man
United na bosi mkubwa Ed Woodward na kuwataka wawe na subira kwa kuwa huenda
mwanzo wa Man U unaweza usiwe mzuri sana.
0 COMMENTS:
Post a Comment