Na Saleh Ally
BURUDANI ya Ligi Kuu England inajuliakana, hata kama
msimu utaisha, lakini unaacha gumzo na rekodi kibao zitakazosimuliwa milele.
Premier League au Premiership inaanza leo, utamu
wake unajulikana lakini machungu yake pia.
Watanzania wengi kama ilivyo sehemu nyingi duniani
watakuwa wanaisubiri ligi hiyo kwa hamu kubwa wakijua kutaandikwa rekodi
nyingine tokea itakapoanza hadi inavyosonga mbele.
Lakini si vizuri kuacha burudani ya rekodi au
matukio ya kuvutia yaliyojitokeza katika msimu wa 2013-14 ambao ulikuwa una
burudani za kila aina.
Kulikuwa na kila aina ya burudani ambayo ilichangia
kuandikwa kwa rekodi mpya kibao ambazo pamoja na kuanza kwa msimu mpya, mpenda
soka yoyote angependa kuzisoma.
Kupitia namba lakini si kwa kufuata moja hadi mia,
badala yake kwa kuchanganya, soka burudani hizo kupitia namba, rekodi ambazo
ziliwekwa huku wachezaji wakiwa hawajui kuwa wanaziweka, badala yake kila mmoja
alipambana kuipa timu yake ushindi.
0
Hakuna hata timu moja ilimaliza msimu bila ya kupoteza hata mechi
moja kama ilivyofanya Arsenal katika msimu wa 1988-89.
1
*likuwa
ni mara ya kwanza mabingwa kumaliza nje ya sita bora tokea msimu wa 1994-95
wakati Blackburn Rovers, wakiwa mabingwa wakamaliza katika nafasi ya saba.
*Huu umekuwa msimu wa kwanza wa Premier League, timu mbili kufunga mabao
zaidi ya 100. Manchester City ilifunga 102, Liverpool wakapachika 101). Msimu
wa 2009-10, Chelsea ilikuwa timu pekee iliyofikisha zaidi ya mabao 100,
ilifunga 103.
*Wakati Adam Johnson alikuwa Mwingereza pekee
aliyefunga hat trick, Marouane
Fellaini alitoa pasi moja tu iliyozaa bao, haladu hakufunga hata moja baada ya
kumaliza msimu wa 2012-13 akiwa ametoa pasi tano za mabao na kufunga 11!
2
Timu
mbili za Liverpool na Fulham, ndiyo zilimaliza msimu bila ya kucheza hata mechi
moja na kupata sare ya 0-0.
4
Beki wa Liverpool, Martin Skrtel ameweka rekodi mpya ya Premiership kwa
kujifunga mabao manne katika msimu mmoja tu.
6
Sunderland
na Liverpool ndiyo timu pekee zilizojifunga mabao sita kila moja.
7
*Bingwa
wa Premier League alipatikana katika mechi ya mwisho kwa mara ya saba katika
misimu 22 mfululizo.
*
Sunderland ndiyo iliongoza kwa kadi nyingi nyekundu baada ya kupata saba.
*Man
United ilipoteza mechi saba za nyumbani, haijawahi kutokea tokea msimu wa
1973-74, halafu ikamaliza ya saba.
8
Daniel
Sturridge alikuwa mchezaji wa kwanza wa Liverpool kufunga mabao katika mechi
nane mfululizo.
10
*Steven
Gerrard alimaliza msimu akiwa na mabao 10, yote ya mikwaju ya penalti.
*Huu ni msimu wa kwanza kuona makocha 10 katika timu
20 za Premier
League wakiachana na timu zao.
12
Liverpool
ilipata penalti 12 ambazo ni nyingi zaidi kuliko za timu nyingine.
13
Manchester
City walifunga mabao 13 kupitia kona wakiongoza kuzidi timu nyingine.
18
Mfungaji kinda zaidi kwenye Premier
League msimu huu alikuwa ni kinda wa Arsenal, Serge Gnabry aliyefunga bao dhidi
ya Swansea akiwa na umri wa miaka 18 na siku 76.
25
Timu
zilibadilishana kukaa kileleni mwa Premier League katika msimu uliopita.
27
Liverpool
ndiyo timu iliyoongoza kwa mashuti ya wachezaji wake kugonga mwaka wa juu
maarufu kama ‘mtambaa wa panya’. Iligongesha mara 27.
31
Luis
Suarez aliyefunga mabao 31, amekuwa mchezaji wa pili kwenye Premier League
kufikisha mabao 30 bila ya mkwaju wa penalti. Wa kwanza alikuwa ni Andy Cole
aliyefanya hivyo katika msimu wa 1993-94 kwa kupachika mabao 34.
32
Romelu
Lukaku ameweka rekodi ya kufunga mabao 32 kwa misimu miwili akiwa mchezaji
aliye kwenye mkopo.
35
Frank
Lampard ndiye mchezaji mzee zaidi aliyefunga bao katika msimu uliopita. Akiwa
na umri wa miaka 35 na siku 289, alifunga bao dhidi ya Stoke, hiyo ilikuwa
Aprili.
59
pamoja
na kutimuliwa, Tim Sherwood ameondoka na rekodi kubwa ya wastani wa ushindi ya
59% ambayo ni ya juu kuliko ya kocha mwingine yoyotr aliyewahi kuifundisha
Tottenham Hotspur kwenye ligi hiyo.
78
Kocha
José Mourinho alipoteza mechi yake ya kwanza akiwa nyumbani kama kocha wa
Chelsea katika mechi mechi yake ya 78 katika Uwanja wa Stamford Bridge.
85
Fulham
imeshikanafasi ya pili kuwa timu iliyofungwa mabao mengi zaidi katika mechi 38
za msimu. Ilipachikwa mabao 85, wanaongoza Derby County ambayo walifungwa 89
katika msimu wa 2007-08.
89
Liverpool
ndiyo timu iliyofanya mabadiliko machache zaidi kuliko timu nyingine kwenye
Premiership msimu huu, ilibadilisha wachezaji mara 89 tu, wakati Chelsea
iliongoza kwa kubadili mara 113.
121
Cheick
Tiote alipiga pasi 121 wakati Newcastle ikiivaa Crystal Palace na kumfanya awe
mchezaji aliyepiga pasi nyingi zaidi zilizofika katika mechi moja kwa msimu wa 2013-14.
999
pamoja
na kumaliza katika nafasi ya saba, Manchester United ilishika nafasi ya kwanza
kwa kupiga krosi nyingi, ilipiga 999 ambazo ni nyingi kuliko zilizopigwa na
timu nyingine yoyote.
0 COMMENTS:
Post a Comment