August 17, 2014


Binti wa bosi wa Simba, Wiam amejumuika na mashabiki wa Liverpool, kuongeza nguvu ya ushangiliaji wakati Liverpool ikiimaliza Southampton kwa kuilaza kwa mabao 2-1 na kuanza vizuri msimu wa ligi.


Wiam aliongozana na baba yake, Musleh Al Ruweh ambaye ni mmoja wa wanachama wa Simba na Liverpool.

Al Ruweh pia ni kiongozi wa Simba ambaye ni mjumbe wa kamati za klabu hiyo. Kama unamkumbuka ndiye yule alitoa zawadi ya gari kwa Ramadhani Singano 'Messi'.

Pia ni kati ya wajumbe wakongwe wa kundi la Friends of Simba na kamera za SALEHJEMBE zilimnasa akiwa kwenye uwanja huo maarufu akiwa na binti yake huyo.
Ushindi huo wa mabao 2-1, umeifanya Liverpool kuanza ligi vizuri dhidi ya Southampton na pia kuamsha morali.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic