August 19, 2014




Unaweza kusema kweli amerejea Premier League, Cesc Fabregas ameshiriki kuzalisha mabao yote matatu wakati Chelsea ilipoitwanga Burnley kwa mabao 3-1 katika mechi yake ya kwanza ya ligi hiyo, usiku wa kuamkia leo.

Fabregas aliyewahi kukipiga Arsenal na baadaye kwenda Barcelona alikoanzia, sasa amerejea katika ligi akiwa na Chelsea.
Bao la kwanza lilifungwa na Diego Costa baada ya yeye kupiga shuti likamgonga beki na kumkuta mfungaji.
Bao la pili lilifungwa na Andre Shurrle baada ya pasi yake tamu na limepewa kuwa bao la wiki.
Halafu bao la tatu likafungwa na beki Branislav Ivanovic akimalizia mkwaju wa kona wa Fabregas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic