August 20, 2014


Gazeti maarufu la michezo la AS la nchini Hispania, limetumia ukurasa mzima kuelezea ziara ya kikosi cha wakongwe cha Real Madrid.
Gazeti hilo limeelezea namna kikosi hicho kinavyofanya ziara kwa mara ya kwanza barani Afrika.
Madrid watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven ambao wameanza kujifua chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa.
Mechi hiyo itapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Madrid wanatarajia kuanza kuwasili kesho.
Kati ya wadhamini wa ziara hiyo na mechi ya kirafiki ni TSN ambao pia ni waratibu wa ziara hiyo, Hoteli ya Sapphire, Bin Slum, Gazeti la Championi na kampuni ya ndege ya Fast Jet.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic