August 24, 2014



Pamoja na kuonekana Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri ni mtaratibu, lakini nidhamu katika kikosi cha Simba imeimarika zaidi.
Kikosi cha Simba kilicho kambini mjini hapa kimekuwa kikifanya mambo yake kwa utaratibu na wachezaji wake wanaonekana kufurahia.
Mazoezi wamekuwa wakifanya kwa juhudi kubwa na kutekeleza yale wanayoelekezwa na kocha wao huyo raia wa Zambia anayesaidiwa na Selemani Matola.
Phiri ni mtaratibu, lakini mara kadhaa amekuwa akiwabadilikia wachezaji wanaoonekana kutokuwa makini.
Awali wachambuzi walieleza kwamba wachezaji wanahitaji mtu ‘mkatili’ au mkorofi kama Zdravko Logarusic aliyetimuliwa.
Lakini inaonekana aina ya kocha kama Phiri atakuwa mfano mzuri kwa kuwa wachezaji ni lahisi kumwelewa na wanatekeleza anayowaelekeza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic