August 24, 2014



Kocha Zdravko Logarusic amesema bado hajafanikiwa kupata ajira mpya.

Loga ameiambia SALEHJEMBE kutoka kwao Croatia, baada ya kufutwa kazi na Simba, sasa anaendelea na mapumziko huku akisubiri ajira mpya.
“Nitaendelea kutafuta na pia kusubiri kama kuna timu zitakuwa zinanihitaji.
“Lakini sasa bado kidogo, hakuna timu wala sina ajira mpya,” alisema Loga akifafanua taarifa za kwamba Gor Mahia ya Kenya imeanza mazungumzo naye.
Loga aliifundisha Simba kwa nusu msimu, lakini baada ya kuingia mkataba mpya wa mwaka mmoja, hakupata nafasi ya kuendelea kuitumikia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic