Mohamed Abdallah, Zanzibar
Andrey Coutinho amefanikiwa kupiga bao na kuisaidia Yanga kuifunga
Shangani inayoshiriki Ligi Daraja la Pili hapa.
Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, moja likiwa
limesababishwa na Salum Telela ambaye alipiga krosi safi mabeki wa Shangani
wakajifunga.
Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa, ilikuwa nzuri nay a kuvutia.
Coutinho alionekana kuwa fiti zaidi huku Mbrazili mwenzake, Jaja
akibanwa.
Yanga ilicheza kwa kuelewana tokea mwanzo, lakini baadaye Shangani nao
walijibu mashambulizi na kuifanya mechi kuwa ya ushindani.
Chini ya Marcio Maximo, Yanga itacheza mechi nyingine moja ya kirafiki
Jumatano kabla ya kurejea jijini Dar.








0 COMMENTS:
Post a Comment