August 20, 2014

FIGO

Mshambuliaji nyota wa zamani wa Real Madrid, Luis Figo amethibitisha kwa mdomo wake kwamba anakuja nchini.

Katika mahojiano kupitia simu, Figo amezungumza na Saleh Ally na kusema anakuja nchini kesho kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.
Lakini akasisitiza, asingependa kuondoka nchini hadi atakapouna Mlima Kilimanjaro.
“Ninafurahi kuja Afrika kucheza, najua kitakuwa kitu kipya na kizuri sana katika maisha ya soka.
“Lakini najua kuhusiana na Mlima Kilimanjaro, nisingependa kuondoka bila ya kuuona Mlima Kilimanjaro.
“Waambie watu waje tufurahie pamoja na Real Madrid imeonyesha inaijali Afrika na Tanzania ndiyo watakuwa wenyeji wetu.”
Hii ni mara ya kwanza Figo kufanya mahojiano moja kwa moja na chombo cha habari.
Figo anawasili nchini kesho usiku akiongozana na kiungo Christian Karembeu raia wa Ufaransa ambaye asili yake ni bara la Afrika.
Mechi hiyo ya Jumamosi, tayari imekuwa gumzo na tiketi zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta vya TSN na maduka ya Supermarket za TSN.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic