FAROUK (KATIKATI) AKIZUNGUMZA HUKU FIGO (KULIA) NA SANZ WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI LEO KATIKA HOTELI YA SOUTHERNSUN JIJINI DAR. |
Mshambuliaji
nyota wa timu ya wakongwe ya Real Madrid, Luis Figo amesema anaiheshimu timu ya
wakongwe ya Tanzania Eleven.
FIGO AKIZUNGUMZA HUKU KAREMBEU, SANZ NA JULIO WAKIMSIKILIZA. KULIA NI MWENYEJI WAO, BOSI MKUBWA KABISA WA TSN, FAROUK BAGHOZA. ALIYESIMAMA NI DENIS SEBBO, MRATIBU WA ZIARA HIYO |
“Lazima
niseme ninaheshimu kikosi cha wakongwe wa Tanzania, tunaamini itakuwa mechi
nzuri nay a ushindani sana,” alisema Figo.
Lakini
kiungo Cristine Karembeu amesema atatoa pasi nyingi kwa Figo ili atumie kipaji
chake na kufunga.
“Unajua
Figo ana kipaji, tutakitumia kwa kumpa pasi nyingi zaidi ili afunge mabao.
“Mechi
haitakuwa lahisi kama alivyosema Figo, ila tunawaomba wasipanie sana ili tutoe
burudani kwa Watanzania,” alisema.
Aidha,
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TSN, Farouk Baghoza amewaomba Watanzania kujitokeza
kwa wingi katika mechi hiyo.
Baghoza
amesema Watanzania watakapojitokeza kwa wingi, itakuwa ni furaha na tiketi
zimeanza kuuzwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment