August 17, 2014




Gumzo la kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata Man United kutoka kwa Swansea kimelifunika jiji la Dar es Salaam.
Gumzo hilo limefanya mashabiki wa Yanga na Simba, kuzisahau kwa muda timu zao za nyumbani na zaidi kujadili kuhusiana na Man United.
Wapenda soka wengi wamekuwa wakizungumzia kipigo hicho kuliko habari nyingine yoyote.

Uchunguzi wa SALEHJEMBE unaonyesha watu wengi wamejadili kuanzia jioni Man United ilipochapwa kwenye mechi ya lipi.
Kwenye email ya blogu hii, mashabiki 1600 walituma ujumbe kulaumu kipigo hicho.
Wengine 2116 walituma ujumbe kwenye akauni ya Facebook ya SALEHJEMBE, wakilalama, wengine wakiunga mkono au kumbeza Kocha Luis van Gaal na wachezaji wake.
Asilimia 16 hadi 20 zilizotumwa zilimuunga mkono au kumkumbushia kocha aliyeyetimuliwa, David Moyes.
Kipigo hicho katika mechi ya ufunguzi ya ligi kimekuwa cha kwanza kwa Man United tokea ilipofungwa mwaka 1972.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic