![]() |
| JAJA, MMOJA WA WACHEZAJI WAPYA WATAKAOONEKANA KWA MARA YA KWANZA KWENYE LIGI KUU BARA. |
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limeongeza kwa siku kumi muda wa kumalizika
usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) kutokana na kuchelewa kwa link ya mfumo mpya wa usajili
(system) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Kwa
mujibu wa CAF, link hiyo itakuwa tayari kwa matumizi ndani ya siku tatu zijazo
kutokana sasa. Hivyo, mameneja wa usajili wa timu hizo kwa sasa wanatakiwa
kukamilisha nyaraka zote zinazotakiwa ili link hiyo itakapokuwa tayari waweze
kuingiza usajili wao mara moja.
Kuanzia
msimu wa 2014/2015 mfumo unaotumika kwa usajili kwa klabu hizo ni wa
elektroniki badala ya ule wa zamani wa kutumia fomu za kawaida. Mfumo huo wa
kisasa ambao pia unatumiwa na CAF unaondoa upungufu uliokuwepo katika mfumo wa
zamani.
Kutokana
na mabadiliko hayo, usajili sasa utamalizika Agosti 27 mwaka huu badala ya leo
(Agosti 17 mwaka huu). Kipindi cha pingamizi ni kuanzia Agosti 28 mwaka huu
hadi Septemba 3 mwaka huu.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana kati ya Septemba 6 na 8 mwaka huu kwa
ajili ya kupitia pingamizi na kuthibitisha usajili.
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inayoshirikisha timu 14 itaanza Septemba 20 mwaka huu
wakati ratiba inatarajia kutoka mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo. Ligi
Daraja la Kwanza inatarajia kuanza wiki ya kwanza ya Oktoba.
Mwisho wa kuombewa Hati ya
Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanatoka nje ya Tanzania ni Septemba
6 mwaka huu.








0 COMMENTS:
Post a Comment