August 17, 2014




Tayari Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri ameungana na kikosi chake mjini Zanzibar.
Simba ilikwenda Zanzibar ikiwa chini ya Selemani Matola ambaye ni kocha msaidizi na kumuacha Phiri jijini Dar.
Lakini leo, kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia ameungana na vijana wake na kuanza kazi.
Phiri alikuwa ameifundisha Simba mara moja tu jijini Dar, mara tu baada ya kusaini mkataba.
“Tayari kocha tuko naye hapa, anaendelea vizuri na kila mtu yuko poa na tumeanza mazoezi,” alisema Matola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic