August 22, 2014



Straika wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu ameweka wazi kuwa, anatumia vidonge maalum kuongeza virutubisho vya mwili ambavyo vinamsaidia kuwa mwepesi na kumudu programu za kocha wake.


Kavumbagu ambaye alikipiga Yanga misimu miwili kwa mafanikio aliyasema hayo hivi karibuni ambapo alikiri kuwa vidonge hivyo vinaongeza virutubisho muhimu mwilini, pia kuulainisha mwili kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi magumu ya kimichezo na si vinginevyo.

“Nimefanya vizuri katika mazoezi kwa kuwa ninapata muda mwingi wa kupumzika na kula chakula katika muda mwafaka, pia kuna rafiki yangu yupo Ulaya amenitumia vidonge f’lani vya vitamin ambavyo nikimeza vinaufanya mwili uwe huru na kuwa tayari kwa ajili ya mazoezi.

“Ni vidonge vya kawaida ambavyo mwanamichezo yeyote anaweza kutumia bila ya kupata madhara, hata Didier Drogba wa Chelsea anavitumia sana,” alisema Kavumbagu.

Alipotafutwa Daktari wa Azam, Mwanandi Mwankenwa juu ya ufafanuzi wa vidonge hivyo, alisema: “Navifahamu vidonge hivyo, vinatumiwa na wachezaji wengi wa Azam, siyo yeye tu, hata (John) Bocco na wengine pia wanatumia, havina madhara kiafya.”

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic