Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limewataka Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kuwa na kiwanja chao cha mazoezi.
Yanga
ambayo ipo kisiwani Pemba kwa ajili ya kambi yake ya kujiandaa na mikikimikiki
ya msimu mpya, inatarajiwa kuwakilisha taifa katika Kombe la Shirikisho Afrika,
lakini imekuwa haina uwanja wa kudumu wa kufanyia mazoezi.
Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema agizo
hilo la Caf limezitaka timu zote za hapa nchini ambazo zitashiriki mashindano
ya kimataifa kuwa na viwanja rasmi vya mazoezi ambavyo vitaweza kutumika muda
wowote.
“Tumepewa
agizo na Caf juu ya kuziambia timu za Azam na Yanga ambazo zitaiwakilisha nchi
yetu kwenye mashindano ya kimataifa kuwa na viwanja vyake rasmi vya mazoezi na
kama timu haitakamilisha agizo hilo, inaweza ikaondolewa kushiriki mashindano
hayo,” alisema Wambura.
Ulipotafutwa
uongozi wa Yanga kulizungumzia hilo, haukupatikana.







0 COMMENTS:
Post a Comment