August 17, 2014



Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri ameamua kikosi chake kuanza mazoezi mara mbili kwa siku.

Leo Simba ikiwa kambini mjini Zanzibar ilifanya mazoezi mara moja tu kwenye ufukwe wa bahati ya Hindi.
Lakini taarifa zimesema kuwa Phiri ameamua sasa kikosi hicho kufanya mazoezi mara mbili kwa wiki.
“Kweli Kocha Phiri amesema kuanzia kesho Jumatatu, mazoezi yatakuwa ni asubuhi na jioni.
“Halafu amesisitiza suala la mechi za kirafiki kwa ajili ya kukiona kikosi,”zilieleza taarifa kutoka kambini Simba.
Phiri amerejea kuinoa Simba baada ya kutimuliwa kwa Zdravko Logarusic.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic