August 18, 2014



Manchester United inajiaandaa kuhakikisha inatenga kitita lundo cha hadi pauni milioni 100 kuhakikisha inamnsa kiungo wa pembeni mwenye kasi kutoka Real Madrid.

Angel di Maria ndiye chaguo la Kocha Louis van Gaal ambaye ameuambia uongozi wa Man United kwamba ufanye kila linalowezekana ili Di Maria atue OT.
Van Gaal amezungumza na bosi mkubwa wa Man United, Ed Woodward na kumuambia azungumze na Madrid kuhusiana na Muargentina huyo.
Iwapo itafanikiwa kumpata, United italazimika kulipa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki. Fedha ambazo wanalipwa nyota wa kikosi hicho kama Wayne Rooney na Robin van Persie.

Tayari United imeanza ligi kwa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Swansea hivyo kufanya van Gaal aanze kuangalia urekebishaji wa makosa yaliyojitokeza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic