August 6, 2014



Kocha Mkuu wa Azam, Joseph Omog, amekisifia kiwango cha mshambuliaji mpya, Didier Kavumbagu, anachokionyesha  kwenye mazoezi ya timu hiyo na kusema anaweza kufika mbali.

Kavumbagu, raia wa Burundi, ni miongoni mwa wachezaji watatu wa kimataifa waliosajiliwa na timu hiyo, akiwemo Ismail Diara kutoka Mali na Lionel Saint-Preux  wa Haiti lakini kocha mkuu wa timu hiyo, amevutiwa zaidi na mchezaji huyo wa Burundi.

 Omog amesema uwezo anaouonyesha mchezaji huyo upo tofauti na wengine kutokana na kuwa ni mtu anayetambua majukumu yake ipasavyo.
“Kavumbagu ni mchezaji mzuri ambaye yupo tofauti na wenzake kwa sababu amekuwa akijituma na kujua nini cha kufanya anapokuwa katika eneo la kufunga pamoja na kusaidia timu inapozidiwa.
“Unajua nilikuwa namfuatilia tangu wakati yupo Yanga ila sasa nipo naye naona uwezo wake halisi, ingawa bado sijapata kikosi cha kwanza ambacho kitakuwa chenye ushindani kutokana na kuwa na wachezaji wengi wazuri,” alisema Omog.

Azam inajiandaa na mchezo wa Ngao ya Matumaini dhidi ya Mtibwa utakaopigwa keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic