August 6, 2014




Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, ameendelea kumkuna kocha mkuu wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo, kutokana na kiwango chake baada ya juzi kufunga mabao mawili mazoezini.


Kocha huyo juzi aliigawa timu yake kwenye vikosi viwili.
Yanga kwa sasa inaendelea na maandalizi yake kwa ajili ya msimu ujao pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Tegete alionekana akifanya vyema kushirikiana na Mbrazil Genilson Santana ‘Jaja’ katika mazoezi yake huku akionekana kubadilika kadiri siku zinavyokwenda.

Hata hivyo, Maximo alisema kuwa anavutiwa na kiwango cha straika huyo kwa sababu siku zinavyokwenda amekuwa akibadilika na kufanya vyema ingawa si yeye pekee ni pamoja na wachezaji wengi wa kikosi hicho ambacho ameanza kukinoa mwezi uliopita.

“Nashukuru viwango vya wachezaji wangu vinabadilika kwa kiasi kikubwa kadiri siku zinavyokwenda na ndiyo kitu ninachohitaji katika kikosi changu, hasa kuwapa nafasi wachezaji wangu washindwe wao wenyewe,” alisema Maximo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic