August 20, 2014

SIWA (KULIA), WAKATI AKIWA YANGA PAMOJA NA MENEJA WAKE, HAFIDH SALEH NA FRED FELIX  MINZIRO.


Aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Yanga, Razack Siwa, hatimaye ameingia mkataba wa kuwanoa makipa wa timu ya Coastal Union ya Tanga.


Coastal Union inajiandaa na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza mwezi ujao.

Siwa ameingia mkataba wa kuwanoa makipa wa timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, lengo likiwa kuipa mafanikio makubwa timu hiyo msimu ujao.

Tayari Siwa ameungana na wachezaji wa timu hiyo leo kupanda ndege kuelekea visiwani Pemba ambako timu hiyo inakwenda kuweka kambi ikijiwinda na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza kabla ya timu hiyo kuondoka, Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi, amesema kuwa kocha huyo wa makipa anachukua nafasi iliyokuwa wazi kutokana na kutokuwa na mwalimu maalumu wa kuwafundisha walinda mlango wa Coastal Union.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic