August 20, 2014

MAXIMO KAZINI.


Na Mohammed Selemani, Pemba
Kocha wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo, juzi alikuwa mkali kwa wachezaji wake ambao walikuwa wakizembea mazoezini.


Yanga ipo hapa kisiwani Pemba kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa baadaye mwezi ujao.

Kocha huyo ambaye alionekana kuwa mkali mara kwa mara, alianza kwa kuwakimbiza wachezaji wake kwa zaidi ya dakika 20 na baadaye kunyoosha viungo kabla hawajaanza kuchezea mpira.

Maximo alionekana kuwa mkali kila mchezaji wake alipokuwa akipoteza mpira kizembe ambapo alimwita na kuongea naye kwa ukali.

Timu hiyo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki kesho ambao utakuwa wa kwanza kwa wachezaji wapya wa timu hiyo kuonekana wakiwa uwanjani wanakipiga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic