August 20, 2014



Mshambuliaji mpya wa Simba, Mkenya Paul ‘Modo’ Kiongera, amesema anaendelea kufanya mazoezi makali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anarejea Simba akiwa katika kiwango cha juu.


Kiongera amekuwa akijaribu kuisaidia timu yake ya KCB kukwepa balaa la kuporomoka daraja katika Ligi Kuu Kenya.

Tayari amesaini mkataba wa miaka miwili na Simba na aliwaonyesha kuwa yuko 'safi' katika mechi ya kirafiki dhidi ya Zesco ya Zambia ambayo Simba ililala kwa mabao 3-0.

“Ninafaya mazoezi vizuri kwa ajili ya majukumu ya hapa Kenya, lakini najua ninakuja Tanzania kuanza kazi na Simba. Lazima niwe fiti zaidi," alisema Kiongera.

Kiongera alipata nafasi hiyo baada ya kuwashinda washambuliaji wengine wawili kutoka Botswana na Gambia ambao walikuwa wanawania nafasi ya kuichezea Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic