August 31, 2014



Kocha Marcio Maximo amesema kikosi chake kinaanza kupata kasi ambayo anaitaka.
Hata hivyo amesisitiza bado anahitaji mechi za kirafiki ili kujipanga vizuri zaidi.
“Lazima kucheza katika mfumo ninaoamini sawasawa, inahitaji mechi nyingine za kirafiki ili kuendelea kujiimarisha.
“Mechi za kirafiki si kwa ajili ya pointi kwa kuwa hii si ligi, lakini ni muhimu kwa maandalizi na kuangalia nini tumefanya kwenye maandalizi kabla ya ligi,” alisema.
Tayari uongozi wa Yanga unalifanyia kazi suala la mechi za kirafiki alizoomba kocha huyo ili kuweka kiwango chake vizuri kabla ya kuanza ligi.
Yanga ilikuwa Pemba na baadaye Unguja ambako ilicheza mechi za kirafiki na kushinda zote.
Lakini bado Mbrazili huyo anataka mechi nyingine jijini Dar es Salaam kujiweka sawa zaidi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic