Msuli wa mshambuliaji mpya
wa Simba, Elius Maguri umekuwa gumzo.
Katika mazoezi ya Simba,
mashabiki wa kikosi hicho wamekuwa wakijadili kuhusiana na miguu yake kuwa na
misuli mingi inayoashiria nguvu.
Mashabiki hao kwenye mazoezi ya Simba huko Boko jijini Dar, wamekuwa
wakijadili kuhusiana na Maguri ambaye amejiunga na Simba akitokea Ruvu
Shooting.
Wengi wamekuwa wakijiuliza
atakavyopambana katika ushindani huo wa namba dhidi ya Amissi Tambwe na Modo
Kiongera kama Simba itafanikiwa kumpata.
0 COMMENTS:
Post a Comment