August 20, 2014



Hatimaye Bodi ya Ligi (PLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wameachia ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2014-14.

Kinachovutia zaidi ni kwamba, watani Yanga na Simba watakutana ‘asubuhiii’, yaani ikiwa ni baada ya kila timu kucheza mechi tatu tu za ligi.
Dar es Salaam derby imepangwa Oktoba 12, ikiwa ni kila baada ya timu kucheza mechi tatu tu.
Kawaida Yanga na Simba hukutana mwishoni mwa mzunguko wa kwanza na ule wa lala salama. Sasa mambo mapema kabisa.
Kabla ya mechi hiyo, Yanga itafungua dimba na Mtibwa Sugar mjini Morogoro wakati Simba itakuwa Dar es Salaam kuwakaribisha Wagosi wa Kaya, Coastal Union.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic