Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid na vigogo wa England wanaosuasua, Manchester
United ndiyo timu zinazomiliki jezi maarufu zaidi za soka duniani.
Madrid na Man United kwa pamoja zimeuza jezi milioni 1.5 ambazo
zimeingiza fedha kwenye klabu hizo.
Maana yake, jezi za klabu hizo zitakuwa zimeuzwa hata mara tatu ya idadi
hiyo kupitia wale ‘wajanja wa mjini’.
Pamoja na wizi, hizo zilizouzwa na fedha kuingia klabuni, zinazifanya
Real Madrid na Man United kuwa klabu zenye jezi maarufu zaidi.
Mauzo hayo ya juu kwa klabu hizo mbili ni tokea msimu wa 2009-10 hadi
ule wa 2013-14
Namba tatu inashikwa na Barcelona ya Hispania halafu Bayern Munich,
Chelsea, Arsenal na Liverpool zinashika nafasi ya nne, hadi saba.
0 COMMENTS:
Post a Comment