Cristiano Ronaldo ameamua kufunguka kuhusiana na uhusiano wake na Kocha
Jose Mourinho na kusema hakuwahi kuwa rafiki yake hata chembe.
Licha ya Mourinho kuwahi kuwa rafiki yake na raia mwenzake wa Ureno,
Ronaldo amesema hajawahi kuwa na urafiki naye, badala yake akasisitiza katika
makocha, rafiki yake ni mmoja tu, Alex Ferguson aliyekuwa naye Manchester
United.
Aidha, Ronaldo amemlaumu Mourinho kwamba wakati akiwa kocha wa Madrid
alisababisha mambo mengi kama ugomvi kati ya wachezaji na hata mashabiki.
Mourinho hakuelewana na Iker Casillas, Angel Di Maria, Sergio Ramos na
hata Mreno mwenzake, Pepe.
Ronaldo amesema Mourinho alifanya hali ya hewa kutotulia ndani ya kikosi
chao huku akisisitiza hayuko kwenye soka kutafuta marafiki, badala yake anataka
kushinda.
0 COMMENTS:
Post a Comment