MANJI (KUSHOTO) AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO. KULIA NI KATIBU MKUU WA YANGA, BENO NJOVU. |
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji, leo ametoa kali kwenye kikao chake na waandishi wa
habari aliposema kwamba ana uwezo wa kuwanuanua wachezaji wa Simba, halafu
wasicheze ligi na badala yake wawe wanafanya mazoezi Covo Beach tu.
Manji
amesema hayo wakati akipinga Simba kutangaza kumsajili mshambuliaji Emmanuel
Okwi.
Manji
amesema suala hilo ni sawa na uhuni kwa kuwa Simba inajua Okwi ana mkataba na
Yanga.
“Kama
itakuwa ni kufanya mambo kwa staili ya kihuni, hata mimi ninaweza kuamua
kuwanunua wachezaji wa Simba sijui kina (Amissi) Tambwe na wenzake, halafu wawe
wanafanya mazoezi Coco Beach tu, wasicheze ligi.
“Lakini
busara ni jambo jema, lakini nione kwamba ninachofanya ni kitu gani na hasara
zake ni zipi.
“Umesikia
sisi (Yanga) tumelalamika kuhusiana na usajili wa Domayo au Kavumbagu kwenda
Azam FC. Kila kitu kilikwenda kwa utaratibu.
“Hata
Simba wanaosema kuhusiana na suala la Okwi pia hawajui, sisi hatukuzozana na
Simba, utaona Okwi wakati anakuja Yanga tulifuata utaratibu na kumalizana na SC
Villa.
“Simba
hawakuwa na tatizo na Okwi, badala yake Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo Yanga
hatukufanya nao biashara. Hakukuwa na sehemu ambayo inatugonganisha,” alisema.
“Sasa
kama kuna lengo la kufanya ili kuikomoa au kuona ni kulipa kisasi, basi ni
kujidanganya tu na kutaka kufanya mambo yaende kwa kukomoana ambalo si jambo
zuri.
“Ndiyo
maana tumetoa siku saba tuwaachie TFF washughulikie madai yetu, ikishindikana,
Caf, Fifa au Cas bado ni sehemu tunazoweza kwenda,” alisisitiza Manji.
“Pia
kusema Okwi amevunja mkataba nasi ni kujidanganya. Iko wapi barua aliyonayo
yeye kwamba tumevunja naye mkataba.
“Hata
majina tumetuma sita, tungejua lipi la kulitoa kwa kuwa hadi Septemba 6 ndiyo
mwisho wa kusajili wageni. Haraka ya nini?”
0 COMMENTS:
Post a Comment