August 25, 2014




Kikosi cha Taifa Stars kitafunga safari kwenda Morocco kukipiga na wenyeji wake katika mechi ya kirafiki ndani ya tarehe za Fifa.

Mechi hiyo imepangwa kuchezwa Septemba 5 nchini Morocco.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Celestine amesema wamepokea mwaliko na tayari Kocha Mart Nooij ameishatangaza kikosi chake.
"Ni tarehe ambayo iko ndani ya tarehe za Fifa, hivyo maandalizi yanaanza na kocha ameishaita kikosi," alisema Mwesigwa ambaye pia ni katibu mkuu wa zamani wa Yanga.
Katika mechi yake ya mwisho, Stars ilichapwa kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini nchini Msumbuji na kutolewa katika mbio za kuwania kucheza michuano ya Mataifa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic