mshambuliaji Mario Balotelli ameamua kuchukua jezi kipenzi chake namba
45 ambayo ataitumia akiwa na Liverpool.
Balotelli amekuwa akiitumia namba 45 tokea akiwa Inter Milan, baadaye
akajiunga na Man City na hata alipokwenda AC Milan.
Jezi hiyo anaamini ndiyo yenye bahati kwa kuwa wakati akiwa kinda
anaichezea Inter Milan, alifunga mabao manne katika mechi nne.
Katika kikosi cha AC Milan, vijana waliochaguliwa kuchezea timu ya
wakubwa huvaa jezi kuanzia namba 36 hadi 45.
Kingine Balotelli ambaye leo atashuhudia mechi kati ya Man City dhidi ya
timu yake mpya ya Liverpool akiwa jukwaani, amekuwa akitania 4+5=9 akiwa ana
maana anavaa jezi namba 9, kijanja.








0 COMMENTS:
Post a Comment