Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa
wachezaji wa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro
ndogondogo klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza
ligi msimu huu wa 2014/2015.
Kasoro hizo ni kufikia makubaliano na klabu ambazo wachezaji
husika wametoka, kuwafanyia uhamisho (transfer) na kulipa ada za uhamisho.
Kamati vilevile ilibaini wachezaji wengi hawakufanyiwa uhamisho kama kanuni za
ligi hizo zinavyoelekeza.
Hivyo, klabu ambazo hazitakuwa zimeondoa kasoro hizo kwa
wachezaji wao leseni zao zitazuiliwa mpaka watakapokuwa wamekamilisha kila
kitu. Ni wachezaji wenye leseni tu ndiyo watakaoruhusiwa kucheza mechi za ligi.
Klabu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Coastal
Union, Kiluvya United, Majimaji, Mji Mkuu, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, Red
Coast na Stand United ziliwawekea pingamizi wachezaji mbalimbali kwa
kutofanyiwa uhamisho.
Kuhusu Ike Bright Obina wa Nigeria aliyewekewa pingamizi na
African Lyon dhidi ya Coastal Union, Kamati imezitaka klabu hizo kufikia
makubaliano, na zikishindwa mchezaji huyo atabaki African Lyon.
0 COMMENTS:
Post a Comment