Kiungo nyota wa Yanga, Coutinho amesema angependa kucheza dhidi
ya Azam FC akiwa fiti.
Coutinho raia wa Brazil ataikosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya
Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, keshokutwa.
Coutinho amesema vizuri kwake kuwa fiti kwa asilimia mia, lakini
kama kuna mashabiki hupendelea kucheza mechi nyingine.
“Ningependa kucheza mechi nyingine kama sitakuwa fiti. Sipendi kulazimisha.
“Usipokuwa fiti, ukacheza mechi, unajiumiza zaidi,” alisema.
Coutinho ataikosa mechi dhidi ya Azam FC kutokana na kuwa
majeruhi.
Aliumia enka katika mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi ya Dar es
Salaam.
Kuumia kwake kunaonekana kuzua hofu kwa mashabiki wa Yanga
katika mechi hiyo dhidi ya Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment