Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) kesho Jumamosi (Septemba 13 mwaka huu) saa 4
asubuhi litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa
mpira wa miguu Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo Uwanja wa Taifa, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na maofisa habari
wa klabu za Azam na Yanga.
Washiriki
wengine wa mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake,
wasimamizi wa milangoni (stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam
maofisa usalama wa TFF.
Mafunzo
hayo yatahitimishwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao ya Jamii
kati ya Azam na Yanga kuanzia saa 10 kamili jioni. Tiketi zimeanza kuuzwa jana
(Alhamisi) kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.
0 COMMENTS:
Post a Comment