Kweli sasa Simba hawana la kusema mbele ya Waganda URA kwa kuwa
wakikutana nao, sawa na mwembe wa uani.
Simba ambao wanapiga pasi nyingi na soka la uhakika wakishinda
mechi yao iliyopita dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, wameshindwa kutamba na kulala
bao 1-0 leo dhidi ya URA.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, URA ndiyo
imeibuka na ushindi na kuendeleza ubabe wake dhidi ya Simba.
Bao pekee Simba lilifungwa na Kalanda Frank katika dakika ya 42.
Juhudi za Simba kusawazisha bao hilo katika kipindi cha pili
ikiwa ni pamoja na kumuingiza Paul Kiongera, lakini wapi, ngoma ikabaki
hiyohiyo moja.
0 COMMENTS:
Post a Comment