NAHODHA WA GLOBAL FC, PHILLIP NKINI EPAFRA AKIZUNGUMZA MBELE YA WACHEZAJI WA KIKOSI CHAKE. |
Timu ya Global FC, keshokutwa Ijumaa
inatarajiwa kushuka dimbani kuwavaa Tegeta Veterani katika mchezo wa kirafiki
utakaopigwa kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Tegeta jijini Dar.
Nahodha wa Global FC, Phillip Nkini, alisema
kuwa mchezo huo ni kipimo tosha kwa kikosi chao kutokana na timu wanayokutana nayo kuwa na wazoefu wengi.
“Tunatarajia kupata upinzani katika mechi hiyo
kutokana na kuwa tutakutana na watu waliocheza ligi kuu kwa muda mrefu, lakini
naamini mchezo huo ni kipimo tosha kwetu kwani kuna mambo mengi tutajifunza
kutoka kwao.
“Ni timu ambayo naifahamu, lakini ukweli ni
kwamba kila mmoja kwenye timu yetu amejiandaa vyema, hatujawahi kufungwa
kirahisi na mechi hii hatutafungwa,” alisema Nkini.
0 COMMENTS:
Post a Comment