PONDAMALI AKIFAFANUA KWA MHARIRI WA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO, PHILLIP NKINI KUHUSIANA NA SUALA LA USHIRIKINA. |
Unaweza
kusema vitu havitokei au ni hadithi tu, lakini wakati mwingine unakutana navyo
kama alivyosema kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali, kuwa uchawi unatumika
kwenye soka naye anauamini.
Pondamali
maarufu kama Mensah amesema uchawi upon a unatumika sana kwenye Ligi Kuu Bara
huku akisisitiza: “Nimesema, andika.”
Pondamali
aliiambia SALEHJEMBE, mbele ya mhariri wa gazeti maarufu la michezo la
Championi Jumatano.
“Nyie
mnapenda sana kuiga uzungu Saleh, uchawi upon a unatumika kwa sana tu.
“Unakumbuka
mimi nilikuwa ninadaka mpira halafu namrudishia mchezaji. Si namponda nao,
namrudishia anapiga tena nanyaka.
“Si
kitu lahisi, najua kazi ni ngumu sana lakini mtaniamini tu. Uchawi ni utamaduni
wa Mwafrika,” alisema.
Alipoulizwa
kama naye pamoja na kuamini ni mtu anayefanya mambo ya kishirikina. Pamoja na
kuonyesha ni amekuwa mkali ghafla, alihoji.
“Mimi
ni Mzungu au Mwafrika, chambua hilo jibu halafu utapata jibu sahihi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment