Kiungo nyota wa Newcastle, Jonas Gutierrez ameamua
kuweka wazi kwamba anapambana na ugonjwa wa kansa unaomtafuna.
Gutierrez amesema alijua anasumbuliwa na ugonjwa huo
baada ya kugongwa na beki Bacary Sagna wakati akiwa Arsenal.
Wakati anachukuliwa vipimo ikajulikana kuwa
anasumbuliwa na kansa.
Alipofanya mahohiano na runinga ya TyC ya kwao
Argentina, kiungo huyo alieleza wazi kuhusiana na hilo.
Kutokana na kuumwa huko, kulisababisha Gutierrez
kusikia maumivu makali ya mara kwa mara na baadaye akatolewa kende lake moja.
Gutierrez ana uwezo wa kucheza kama kiungo au beki wa kushoto.
Hali yake hiyo imewaikitosha watu wengi sana hasa
baada ya kusikia ni mgonjwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment