September 17, 2014

LEONEL (KUSHOTO) AKIONGEMBEA MPIRA NA JUMA ABDUL WA YANGA.

Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Azam FC, Mu-ivory, Coast Kipre Tchetche, amesema anaamini kombinesheni waliyoitengeza na mastraika wengine kikosini hapo itakuwa ya hatari na ya kuvutia msimu ujao.
Tchetche amesema kuwa uwepo wa Mrundi Didier Kavumbagu na Mhaiti Leonel Saint-Preux, unatosha kabisa kuifanya safu yao ya ushambuliaji kuwa kali, hasa ukizingatia tayari wameanza kuelewana na kujua wacheze vipi ili waweze kuivuruga ngome ya timu pinzani.
“Kwa sasa tuna safu nzuri ya ushambuliaji, najua Kavumbagu na Leonel ni wageni Azam, lakini wana viwango vikubwa, tumeweza kufanya mazoezi kwa miezi michache tuliyokuwa pamoja na tumeshaanza kujuana.
“Najua ni jinsi gani nicheze na Leonel na jinsi gani nicheze na Kavumbagu ili tuweze kufunga, hata wao pia wanajua wanaweza kushirikiana na mimi vipi uwanjani mpaka tuweze kufunga, naamini tutakuwa moja ya safu nzuri za ushambuliaji msimu ujao.”

Hata hivyo, Tchetche alipoulizwa kuhusu mechi ya Ngao ya Hisani, waliyofungwa na Yanga kwa mabao 3-0 wikiendi iliyopita, alisema: “Ilikuwa si bahati yetu au pengine tulizidiwa maarifa lakini tulijitahidi na matokeo ndiyo yakawa kama yalivyotokea.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic