September 3, 2014



Na Saleh Ally
REKODI zilizopatikana kutokana na usajili wa ligi mbalimbali za Ulaya umekuwa ukipishana lakini kwa idadi ndogo sana na hii inatokana na vyombo vya habari au wale wanaozitoa kwao wanavyowahabarisha.


Lakini haziondoi suala la kuonyesha hali halisi, mfano BBC inaamini England kwa usajili wametumia kitita cha pauni milioni 835 na Dailymail wanaamini ni pauni milioni 857.7, hii inaonyesha hakuna tofauti kubwa sana.

Kikubwa cha kujadili ni namna ambavyo England imeingia kwenye njia nyingine kabisa kutokana na timu zake kutumia idadi kubwa ya fedha katika usajili hadi kufikia kuzitupa mbali ligi za Hispania ‘La Liga’ na Italia ‘Serie A’ ambazo zimekuwa ziking’ara kutokana na kutumia fedha nyingi katika usajili.

 Katika kipindi cha misimu miwili, klabu za England, Tottenham Hotspur na Liverpool ziliwauza Gareth Bale na Luiz Suarez kwa vigogo wa Hispania, Real Madrid na Barcelona.

Hadi sasa biashara ya Bale ndiyo uhamisho ghali zaidi kwa kuwa aliuzwa kwa pauni milioni 85, Suarez naye ni kati ya uhamisho ghali kwa kuwa ni pauni milioni 75.

Msimu uliopita wa 2013-14, klabu za England zilitumia pauni milioni 760, lakini msimu huu gharama zimepanda maradufu hadi kufikia pauni milioni 857 ambayo imevunja rekodi ya misimu yote tangu kuanzishwa kwa ligi hiyo.

Misimu miwili sasa, Premier League imebadilika, badala ya kuuza wachezaji tu Hispania imekuwa ikinunua tena kutoka La Liga na kwa bei ghali.

Arsenal imefanya hivyo misimu miwili mfululizo ikianza kumnunua Mesut Ozil kutoka Real Madrid na msimu huu ikamnunua Alexis Sanchez kutoka Barcelona wakati Man United ilimtwaa Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao, kisha ikamnasa Angel Di Maria kutoka Real.

Lakini hiyo haitoshi, Premier League sasa ndiyo ligi ghali zaidi kutokana na kutumia fedha nyingi za usajili mara mbili ya La Liga ambayo inashika nafasi ya pili.

Usajili wa La Liga ambayo inawajumuisha vigogo Real Madrid na Barcelona, umegharimu zaidi ya pauni milioni 434 wakati Serie A ina pauni milioni 272 zilizotumika kwa ajili ya manunuzi ya uhamisho wa wachezaji.

 Bundesliga yenyewe imetumia pauni milioni 261 wakati Ufaransa kupitia klabu zao mbili kubwa, angalau walijisukuma na kufikia hadi pauni milioni 112.

Hii utaona kiasi gani Premier League imegeuka kuwa ligi maarufu lakini pia inayotumia fedha nyingi na zaidi klabu tano za juu ndizo zimetumia fedha nyingi.

Manchester United ndiyo imeongoza kwa kumwaga pauni milioni 153.1, Liverpool inafuatia kwa kutumia pauni milioni 116.8, Chelsea (pauni milioni 87.7), Arsenal (pauni milioni 78.2), Southampton (pauni milioni 57.9) na Man City (pauni milioni 54.5).


Mara chache sana usajili kushuka, lakini kutokana na fedha hizo za kiwango cha juu zinazotumika, Premier League itazidi kuwa ligi maarufu zaidi duniani kwa asilimia 63 badala ya 58 ilizokuwanazo awali.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic