Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali
amesema amefurahishwa na ujasiri wa klabu za Mbeya City na Ndanda FC kufanya
uamuzi wa kusherekea siku zao maalum.
Tiimu hizo zilifanya Mbeya Day na Ndanda Day,
hali ambayo Dalali ambaye ni mwanzilishi wa Simba Day ameziita ni uamuzi wa
kijasiri.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Dalali alisema uamuzi
wa klabu hizo mbili ulikuwa sahihi.
“Ni sahihi kabisa, hakukuwa na sababu ya kuingia
hofu ya aibu kama wakifanya itaonekana kitu ni cha kuiga.
“Kama una jambo zuri vizuri kufuatisha, kwa kuwa
Ndanda na Mbeya City wamefanya hivyo, basin a timu nyingine ziige ili kuongeza
utamu wa suala hili,” alisema Dalali.
Dalali alikuwa kati ya waalikwa wa Ndanda Day
mjini Mtwara na aliongozana na mwenyekiti wa sasa wa Simba, Evavs Elieza Aveva.
0 COMMENTS:
Post a Comment