KALI ALIYEWAHI KUICHEZEA YANGA AKISALIMIANA NA KOCHA WA YANGA, MARCIO MAXIMO WAKATI WA MECHI YA NGAO YA JAMII, JUMAPILI ILIYOPITA. |
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala, ameukubali uwezo wa Mbrazili, Geilson Santos
Santana ‘Jaja’ wa Yanga na akasema wazi kuwa wanaompinga wanamuonea na hawajui
uzuri wa mchezaji kama huyo kikosini.
Kauli
ya kocha huyo inakuja baada ya kuwepo kwa maneno mbalimbali kuhusu straika huyo
aliyetupia mabao mawili juzi na kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
dhidi ya Azam kuwa si chaguo sahihi kwa Yanga kwa ajili ya msimu ujao kutokana
na staili ya uchezaji wake.
Ongala aliyewahi kuwa mshambuliaji hatari wa Abajalo ya Sinza na Yanga alifafanua kuwa Watanzania walio wengi wanapenda wachezaji wenye spidi na
chenga nyingi kama Mrisho Ngassa na hawapendi kumuona mchezaji mwenye kutulia
uwanjani na kufanya kilichomleta, ndiyo maana hawaelewi umuhimu wa wachezaji
kama Jaja wanapokuwa uwanjani.
“Wengi
wanapenda mchezaji mwenye spidi na vyenga vingi kama Mrisho Ngassa, sasa si
kila mchezaji yupo hivyo, kwa sababu kila mtu ana silaha yake aliyojaaliwa nayo
kwenye soka. Jaja ni straika na kazi yake iliyomleta uwanjani ni kufunga, hayo
mambo mengine watafanya wengine.
“Kwangu
mimi Jaja ni mchezaji mzuri na anayeijua kazi yake na ana msaada kwa timu kwa
sababu anafanya kitu muhimu zaidi katika matokeo ya mechi. Mimi nawashangaa
sana wanaomlaumu eti hajui mpira au hana msaada kwa timu kutokana na staili
yake ya uchezaji.
“Wanashindwa
kuelewa na kujua umuhimu wake, ndiyo maana wanamlaumu pasipo sababu ya maana,
nafikiri wangetulia tu ili Jaja afanye kazi yake ya kufunga pekee anayoifahamu
na kuipa faida timu.”
Jaja
amesajiliwa Yanga hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili na tayari
amefanikiwa kufunga mabao matano ndani ya mechi tano alizoichezea timu hiyo,
zikiwamo nne za kirafiki na moja dhidi ya Azam wikiendi iliyopita.
0 COMMENTS:
Post a Comment