Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah
Kibadeni, amesema mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel
Okwi, anateswa na mzimu wa marehemu, Patrick Mafisango kwa kuwa ndiye aliyekuwa
akimchezesha.
Okwi amesajiliwa na Simba katika dakika za
mwisho lakini alikuwa hajaonyesha ubora wake kwenye mechi za kirafiki
alizocheza kabla ya jana kuivaa Coastal.
Kibadeni
amesema Okwi anahitaji ajipange ipasavyo ili aweze kupata nafasi ya kucheza
Simba na kumpata mtu wa kumchezesha kama ilivyokuwa kwa Mafisango ambaye ndiye
aliyekuwa msaada mkubwa kwake.
“Okwi ninayemjua mimi si huyu wa sasa kwani
kiwango chake kimeshuka mno, hivyo anahitaji kujipanga ipasavyo kwa kuonyesha
juhudi za hali ya juu ili aweze kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.
“Zamani wakati anaichezea timu hiyo alikuwa na
mtu wa kumchezesha, marehemu Mafisango, hivyo kwa sasa anahitaji mtu mwingine
aweze kumchezesha na kuwa katika kiwango kizuri kama cha awali,” alisema
Kibadeni.
0 COMMENTS:
Post a Comment