Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed, amesema alitumia
karibu wiki nzima kuyasoma mabao ya straika wa Yanga, Geilson Santos ‘Jaja’ ili
amzuie asilete madhara langoni mwake.
Mbinu hiyo ya Mohammed ambaye aliwahi
kuichezea Yanga, ilizaa matunda kwani aliokoa penalti ya Mbrazili huyo pamoja na
michomo mingine hatari katika mchezo wa Ligi Kuu Bara baina ya timu hizo, juzi
kwenye Uwanja wa Jamhuri, Moro.
Mohammed alishtushwa na uwezo wa Jaja mara
baada ya kumtungua kipa wa Azam FC, Mwadin Ally kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii
wiki moja iliyopita, ndiyo akaamua kumfungia kazi.
Kipa huyo ambaye inaaminika ndiye alikuwa nyota
wa mchezo wa juzi, alisema: “Ukweli hilo liliniongezea umakini kama ulivyoona
nilivyokuwa nikimchukulia mipira eneo la hatari.”
Mohammed pia amewahi kuichezea Majimaji ya
Songea ambayo hivi sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment