Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, amewataka
mashabiki wa timu hiyo kutokatishwa tamaa na matokeo ya mchezo wa juzi Jumamosi
wa ligi kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri,
mjini hapa na timu yake kupokea kipigo cha mabao 2-0.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Maximo
alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu na wachezaji wake walipambana hadi dakika ya
mwisho lakini bahati haikuwa yao.
Maximo alisema sasa anajipanga upya kuelekea
mchezo ujao na anaamini Yanga itafanya vizuri katika ligi hiyo.
“Mpira ndivyo ulivyo, siku nyingine inakuwa
ndiyo na wakati mwingine inakuwa hapana,” alisema.
Hata hivyo, kocha huyo alilalamikia hali ya
Uwanja wa Jamhuri kuwa si nzuri na iliharibu mipango mingi ya wachezaji wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment