Mshambuliaji mpya wa Simba, Paul Kiongera jana alilazimika kucheza dakika chache tu baada ya kuingia, halafu akatolewa tena.
Kiongera alitolewa baada ya kuumia ikiwa ni kutokana na kugongana na kipa Shabani Kado wa Coastal Union na inaonyesha alinusurika kwa kuwa angeweza kuumia vibaya zaidi.
Baada ya kugongana na Kado katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2, Kiongera aliangukia vibaya shingo.
Hata hivyo imeelezwa anaendelea vizuri na hajapata madhara makubwa sana hasa shingoni au kichwani. Cheki picha zote tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment