Kocha Mkuu wa Prisons ya
Mbeya, David Mwamwaja amesema wanataka kuendeleza vipigo kwa lengo la
kujiimarisha kileleni.
Mwamwaja aliyewahi kuinoa
Simba, amesema ushindi wao wa kwanza wa ligi katika mechi ya kwanza, umewapa
nguvu za kutaka kuendelea kujikusantia pointi tatu.
Prisons iliichapa Ruvu
Shooting kwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa
Mabatini Mlandizi, Pwani.
“Mechi ilikuwa ngumu lakini
tumefurahia kushinda. Tunataka kushinda zaidi na tumeanza kucheza mechi kadhaa
za kirafiki kujiimarisha.
“Tutacheza na Ashanti iliyo
daraja la kwanza kama kujiweka sawa zaidi. Halafu tutarudi kwenye ligi kutafuta
ushindi zaidi.
“Unaposhinda mapema mapema,
unajiweka vizuri na kuepuesha presha mwishoni mwa ligi ambako siku zote
kunakuwa pagumu,” aliongeza Mwamwaja.
0 COMMENTS:
Post a Comment