Mashabiki wa Simba mjini hapa walimvamia mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, wakitaka kupiga naye picha.
Hali hiyo ilisababisha vurugu kubwa hadi kulazimika kwa askari polisi zaidi ya wanne kuingilia kati kuongeza ulinzi.
Simba ilikuwa mkoani hapa kucheza mechi ya
kirafiki dhidi ya Ndanda katika kuadhimisha Siku ya Ndanda (Ndanda Day). Mchezo
ulipigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona na kumalizika kwa sare ya 0-0.
Okwi, raia wa Uganda, alivamiwa na kundi kubwa
la mashabiki hao uwanjani baada ya mechi kumalizika, hali iliyowalazimu askari
polisi watano waliokuwa na silaha, kuingilia kati kumuokoa.
SALEHJEMBE lilishuhudia Mganda huyo akitolewa
uwanjani nchini ya ulinzi mkali wa askari hao ambao walikuwa wamebeba silaha za
mabomu ya machozi na kumuingiza kwenye vyumba vya wachezaji.
Wakati mshambuliaji huyo akipelekwa vyumbani,
kundi lingine liliibuka na kwenda kumvaa kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia,
Patrick Phiri kwa malengo ya kupiga naye picha pamoja na kumsalimia lakini
polisi waliwahi kumuokoa.
Hata hivyo kutokana na kila mmoja kutoka kipiga picha kwa wakati mmoja, ikawa kama vurugu tena, polisi wakalazimika kuingilia kwa mara nyingine na kumuondoa eneo hilo huku wakitishia kutembeza kichapo.
0 COMMENTS:
Post a Comment